Friday, March 25, 2011

Fahamu unakokwenda

Safari. Hupangwa


Bila shaka umewahi kusafiri


Pengine katika moja ya safari zako umewahi kujilaumu
lakini zipo ambazo umewahi kuzifurahia sana


Zipo pia hutaki hataki hata kuzikumbuka jinsi ulivyopata taabu na misukusuko njiani. Zipo pia ulizonusurika kuumia ajalini.
Zote ni safari.

Soma hadithi hii ya akina dada wawili.
Siku moja Nia na Tumaini waliamua kufanya ziara ya jiji. 
Safari hii waliamua tangu mapema tu asubuhi, ambapo Nia alimuarifu Tumaini kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi; " mambo Tuma, nitakupitia hapo kwenu twende tukatembee  leo". Ulisomeka ujumbe wa Nia kwa Tumaini. 

Tumaini alipoupata pasi na kuchelewa alimjibu Tumaini;
" mambo safi, haina shida best nitakuwepo tu nipitie". 

Hatimaye muda wa safari uliwadia na siku hiyo waliamua watumie usafiri wa Taxi. Wakiwa kwenye Taxi safari ikiwa tayari imeanza, dereva aliwauliza " mnaelekea wapi kina dada?". 

Ghafla Tumaini na Nia wakaangua vicheko. "Hivi kweli tunaelekea wapi" akaulizaa Nia. swali hilo lilimshtua Tumaini na akauliza pia '' ah mi nilifikiri unajua tunakoelekea?"  

Yule dreva Taxi naye kwa mshangao akauliza " sasa kama hamjui mnakoenda nitawafikishaje?" 

Dada, ule msemo unaosema maisha ni safari. Ni kweli. Kwa asilimia kubwa maisha ni sawa na safari. 


Huwezi kufika unakotaka kwenda kama hujaamua unakwenda wapi. Nini hasa malengo yako? zipi ndoto zako? familia? elimu? kazi nzuri? kabla hujaanza safari panga kwanza unakokwenda.

Hakikisha umejiandaa vya kutosha na kuchukua kila unachohitaji. kisha tafakari juu ya njia unayotaka kutumia ndio sahihi? utafika salama? kwa sababu kama hujui wapi unataka kufika kimaisha basi ni rahisi kujikuta umefika mahali kwingine kabisa. Panga maisha yako.





 
Dada. Furahia kila dakika.

   

Thursday, March 24, 2011

Dakika Tano na Dada Furahia kila dakika


Maalum kwa ajili ya mijadala, ushauri na maswali. Dakika Tano na Dada inalenga kuwapatia akina dada, marafiki, akina mama uwanja wa kujadili masuala mbalimbali wanayokutana nayo katika maisha yao ya kila siku hususan namna ya kuwalea na kuwakuza watoto wetu wadogo tangu siku ya kwanza, changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo lakini wakati mwingine wanahisi wanalemewa. Karibu mama utupe uzoefu wako!


Kupitia jukwaa hili utarajie kupata faraja na matumaini mapya katika yale ambayo unadhani yamekuwa yakikusumbua moyoni na hujui nani wa kuumuuliza. Ukiwa kama wewe ni binti unayekuwa unahitaji kupata msaada wa wazazi, rafiki na majirani lakini pengine kutokana na mazingira ya ukuaji wako hali hiyo unashindwa kumkabili mama au baba au yeyote nyumbani kumueleza juu ya hisia zako. Ufanye nini basi unapohisi umezongwa na kitu? ufanye nini endapo unahisi unahitaji kuanzisha mahusiano? Karibu binti upate mwongozo!



Dakika Tano na Dada itakuimarisha na kukufanya ufurahie kila dakika.


Karibu!