Bila shaka umewahi kusafiri
Pengine katika moja ya safari zako umewahi kujilaumu
lakini zipo ambazo umewahi kuzifurahia sana
Zipo pia hutaki hataki hata kuzikumbuka jinsi ulivyopata taabu na misukusuko njiani. Zipo pia ulizonusurika kuumia ajalini.
Zote ni safari.
Soma hadithi hii ya akina dada wawili.
Siku moja Nia na Tumaini waliamua kufanya ziara ya jiji.
Safari hii waliamua tangu mapema tu asubuhi, ambapo Nia alimuarifu Tumaini kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi; " mambo Tuma, nitakupitia hapo kwenu twende tukatembee leo". Ulisomeka ujumbe wa Nia kwa Tumaini.
Tumaini alipoupata pasi na kuchelewa alimjibu Tumaini;
" mambo safi, haina shida best nitakuwepo tu nipitie".
Hatimaye muda wa safari uliwadia na siku hiyo waliamua watumie usafiri wa Taxi. Wakiwa kwenye Taxi safari ikiwa tayari imeanza, dereva aliwauliza " mnaelekea wapi kina dada?".
Ghafla Tumaini na Nia wakaangua vicheko. "Hivi kweli tunaelekea wapi" akaulizaa Nia. swali hilo lilimshtua Tumaini na akauliza pia '' ah mi nilifikiri unajua tunakoelekea?"
Yule dreva Taxi naye kwa mshangao akauliza " sasa kama hamjui mnakoenda nitawafikishaje?"
Dada, ule msemo unaosema maisha ni safari. Ni kweli. Kwa asilimia kubwa maisha ni sawa na safari.
Huwezi kufika unakotaka kwenda kama hujaamua unakwenda wapi. Nini hasa malengo yako? zipi ndoto zako? familia? elimu? kazi nzuri? kabla hujaanza safari panga kwanza unakokwenda.
Hakikisha umejiandaa vya kutosha na kuchukua kila unachohitaji. kisha tafakari juu ya njia unayotaka kutumia ndio sahihi? utafika salama? kwa sababu kama hujui wapi unataka kufika kimaisha basi ni rahisi kujikuta umefika mahali kwingine kabisa. Panga maisha yako.
Dada. Furahia kila dakika.


No comments:
Post a Comment